Friday, June 22, 2012

TPSF yatoa bilioni 5.5 kwa wajasiriamali

Godfrey Simbeye, Mkurungenzi TPSF


Mfuko wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania ‘TPSF’ imetoa shilingi bilioni tano na nusu kwa wajasiliamali waliopata alama za juu katika mafunzo ya kuwajengea uwezo kwa lengo la kujiendeleza katika kujikwamua na umaskini.

Jumla ya wajasiliamali 1565 kutoka katika mikoa ya Tanzania bara na visiwani wamepata mafunzo hayo huku kati yao wanawake wakiwa ni 56%  na vijana walio na umri chini ya miaka 35 wakiwa ni 43%.
Mkurugenzi mtendaji wa TPSF Godfrey Simbeye amesema tayari faida imeanza kuonekana kutokana na wajasiliamali hao kuanza kujitegemea.

No comments:

Post a Comment