Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni
400 kwa ajili ya kuziwezesha kaya
masikini katika Wilaya tatu za Kibaha, Bagamoyo na Chamwino ikiwa ni awamu ya tatu ya utekelezaji wa
mpango wa maendeleo unaosimamiwa na Mfuko wa maendeleo ya jamii Tanzania TASAF.
Mpango huo ambao ulianza kwa majaribio katika
Wilaya hizo kuanzia mwaka 2005,unaelezwa kuleta mafanikio kutokana na
kuziwezesha kaya masikini ambazo zinaongozwa na Wazee,watoto na wajane ambapo
Fedha hizo zimetolewa kwa ushirikiano wa Bank ya Dunia,Shirika la maendeleo la
Uingereza DFID na Serikali ya Hispania.
No comments:
Post a Comment