Thursday, June 28, 2012

Airtel wachangia damu



Hawa Bayuni


Wafanyakazi wa kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel leo wamejitolea kwa hiari kuchangia damu ili kusaidia kitengo cha damu salama kinachohudumia wananchi wenye upungufu wa damu.
Mwezi june kila mwaka hujulikana kama mwezi wa kujitolea damu ambapo watu mbalimbali wanahimizwa kuchangia damu kwa hiari yao ili kuiwezesha benki ya damu kuwa na akiba ya kutosha ya damu.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa kampuni hiyo Hawa Bayuni kutoka kitengo cha utawala amesema wao kama wafanyakazi wameungana na watanzania wengine kuchangia damu kwa Benki ya Damu nchini ili kuiwezesha kuwahudumia watanzania.
Kitengo hicho cha benki ya damu kilicho chini ya ofisi ya wizara ya afya kinahitaji lita 200 za damu ili iweze kuhudumia wagonjwa waohitaji huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment