Saturday, June 23, 2012

Serikali ya Zambia yatenga Dola Milioni 10 kwa ajili ya Tazara


Panji Kaunda, Naibu Waziri wa Uchukuzi Zambia

Baadhi ya wafanyabiashara walioudhuria mkutano huo

Baadhi ya wafanyabiashara walioudhuria mkutano huo


Serikali ya Zambia imetenga jumla ya Dola Milioni 10 kwa ajili ya uboreshaji wa Shirika la Reli ya Tazara pamoja na changamoto mbalimbali zinazolikabili shirika hilo.


Naibu Waziri wa Uchukuzi wa Zambia Bwana Panji Kaunda amethibitisha hilo leo jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano mkuu kati ya wafanyakazi wa Shirika hilo na Wafanyabiashara wakubwa wanaosafirisha bidhaa zao kwa kutumia Reli ya Tazara.
Waziri Kaunda amesema pia kuwa ni wajibu wa serikali zote mbili kati ya Tanzania na Zambia kuboresha mahusiano mazuri kwa kuwekeza katika shirika hilo ili kuwavutia wafanyabiashara kuendelea kusafirisha bidhaa zao na hatimaye kukuza uchumi wa nchi hizo. 

Naye katibu wa wizara ya uchukuzi nchini Tanzania Bwana Omary Chambo amesema hii ni mara ya kwanza kwa nchi ya Zambia kutenga bajeti kwa ajili ya shirika hilo. Nao baadhi ya wafanyabiaashara wamezitaka nchi zote mbili Tanzania na Zambia kuboresha miundombinu ya shirika hilo ikiwemo mishahara ya wafanyakazi ili kupunguza migogoro baina ya wafanyakazi na Serikali.


No comments:

Post a Comment