Saturday, June 23, 2012

Mimba Mashuleni yaathiri kiwango cha elimu Kishapu



Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu



Tatizo la mimba mashuleni kwa  Wakazi wa Kata ya Songwa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga linadaiwa kuathiri kiwango cha elimu kwa watoto wa kike kutokana na umaskini katika maeneo wanayoishi.



Bi Rachel Mdundo kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP ngazi ya Jamii  amesema kuwa utafiti uliofanywa katika kipindi cha mwaka 2011 pekee umebaini kuwa wanafunzi 31 wa kata ya Songwa wamepata ujauzito na kusababisha kukatiza masomo yao.

Naye Bi Jamila Nyalulu ambaye ni mmoja wa wazazi katika Wilaya hiyo  anasema kumekuwapo na tabia za wazazi kuwaamuru watoto kutofanya vizuri makusudi katika mitihani yao ili wafeli kwa kigezo cha kuwasaidia kazi za nyumbani hatua inayodidimiza sekta ya elimu wilayani hapo; kauli ambayo inaungwa mkono na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Injinia Lucas Said ambaye anasema amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wanafunzi kuhusiana na hatua hiyo na kuahidi kulifanyia uchunguzi suala hilo ili sheria ishike mkondo wake.
 


Kumekuwa na chamgamoto mbalimbali zinazohusu elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mojawapo ikiwa ni mimba mashuleni,vifaa vya kufundishia,nyumba za walimu na mengine mengi,jitihada za haraka zinahitajika ili kuweza kuinusuru hali hiyo.



No comments:

Post a Comment