Friday, June 22, 2012

Sekta ya afya inakabiliwa na uhaba wa wataalam wa mahabara






 
Serikali inakabiliwa na uhaba wa wahudumu wa fani ya maabara hali inayochangia kuzorota huduma hiyo katika baadhi ya vituo vya afya nchini.

Hali hiyo imebainishwa na Bw.Dickson Majige ambaye ni Mkuu wa huduma za maabara nchini wakati wa maadhimisho ya huduma za maabara.

Nao baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Uuguzi na Tiba katika Hospitali  hiyo walioshiriki maadhimisho hayo wakaitaka serikali kuboresha mazingira ya kazi na kuwaongezea vitendea kazi.

Maadhimisho hayo yemefanyika ili kuangalia changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya kwa upande wa maabara na kuifikishia serikali ili izifanyie kazi.

No comments:

Post a Comment