Shilingi milioni 560 zinatarajiwa kuchangishwa kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa vifaa vya hospitali katika wodi ya wagonjwa wa saratani kwa watoto ambayo itajengwa katika hospitali ya taifa ya muhimbili iliyopo jijini dar es salaam.
Tayari ujenzi wa hospital hiyo umeanza kufanyika ambapo upo katika ngazi ya uchoraji wa ramani ambao ujenzi mzima utagharimu shilingi million 750 na itakuwa na ubora mkubwa kuliko nchi nyingine yeyote kusini mwa jangwa la sahara.
Taasisi ya kusaidia jamii ya Rotary Club kwa kushirikiana na wafadhili mbalimbali wameandaa mbio za hisani zitakazo shirikisha zaidi ya wakimbiaji 5000 kwa lengo la kuchangisha fedha hizo na baadaye kuzitumia kwa ununuzi wa vifaa hivyo vya hospitali.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa bodi ya benki ya Bank M Nimrod Mkono amesema kuwa jengo hilo litakuwa bora zaidi na litasaidia kwa kiasi kikubwa kutibu wagonjwa wa saratani nchini.
Naye mwenyekiti wa mbio hizo ambazo zitafanyika siku ya Kumbukumbu ya siku ya kifo cha baba wa Taifa mwalimu Kambarage nyerere mwezi Octoba Zainul Dossa amesema kuwa lengo ni kuhakikisha taasisi yake inawafikia wananchi wenye mahitaji mbalimbali ambao kwa kiasi kikubwa hawana uwezo wa kifedha,
Taasisi hiyo ambayo ina miaka 4 nchini mwaka 2010 ilichangisha million 140 na kusaidia ujenzi wa visima kwa ajili ya wanafunzi wa shule mbalimbali na mwaka 2011 walichangisha fedha milioni 750 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wagonjwa wa saratani kwa watoto.
No comments:
Post a Comment