Baadhi ya wateja wa benki
ya NMB wameendelea kujipatia zawadi mbalimbali ikiwemo Tani moja ya mifuko ya
Cement pamoja na Mabati kupitia bahati nasibu inayoendeshwa na benki hiyo
ijulikanayo kama Jenga Maisha Bora.
Akiongea wakati wa
kukabidhi zawadi hizo Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo
Imani Kajula amesema kuwa wameamua kuanzisha bahati nasibu hiyo ili kuwajengea
wananchi tabia ya kujiwekea akiba.
Baadhi ya wateja
walioibuka na ushindi huo wamewataka wananchi kuachana na tabia ya kuweka fedha
katika majumba yao na badala yake
wapende kujiwekea akiba za fedha zao katika mabenki.
Jumla ya wateja watano
wameibuka na ushindi huo akiwemo Richard makala, Edgar Mandera, Zariah Sarungi
na Ramadhan Mgunya wakazi wa jiji la Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment