Siku moja baada ya Rais
Jakaya Kikwete kuwataka madaktari walio kwenye mgomo kurejea kazini na
kuwahudmia wagonjwa, Madaktari Bingwa nchini wametangaza mgomo na kusema liwalo
na liwe.
Mgomo huo ambao unaonekana
kuwa wa kimaslahi zaidi unaonekana kushika kasi kila uchao tofauti na
ilivyokuwa mwanzoni mwa wiki iliyopita.
Kiongozi wa Madaktari Bingwa
Dr Catherine Mng’ong’o amewaambia waandishi wa habari Jijini Dar es salaam kuwa
baada ya kikao chao cha Jumatatu, wamekubaliana kuendelea na mgomo wa nchi
nzima.
Dr Mng’ong’o amesema,
hawawezi kuendelea na kazi kwa vitisho vya serikali huku wenzao wakifukuzwa
bila taratibu na hivyo wameamua kuendelea na mgomo wao.
Edwin Chitage ni katibu wa
jumuiya ya madaktari nchini ambaye anasema wamesikitishwa na kauli hiyo ya
Rais na kutaka suluhu ya mezani zaidi kumaliza mgogoro huo.
No comments:
Post a Comment