Wednesday, July 4, 2012

HUDUMA ZAENDELEA KUTOLEWA MOI


BODI YA WADHAMINI WA KITENGO CHA MIFUPA –MOI- IMETANGAZA  KUENDELEA KWA HUDUMA ZAKE KAMA KAWAIDA.

KATIKA MAONGEZI NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA KITENGO CHA MIFUPA CHA MOI BALOZI  CHARLES MUTALEMWA AMBAYE NI MWENYEKITI WA BODI HIYO YA MADAKTARI AMESEMA MADAKTARI WOTE 61 WA MOI WAMETHIBITISHA  KUENDELEA NA KAZI.

MUTALEMWA AMEFAFANUA KUWA WAKATI WOTE WA MGOMO MADAKTIRI BINGWA 18 WA MOI WALIENDELEA KUTOA HUDUMA ZA DHARURA

MNAMO TAREHE 29 JUNE BODI HIYO ILIFANYA KIKAO CHA DHARURA AMBAPO ILIWASIHI MADAKTIRI WA MOI KUITIKIA WITO WA SERIKALI NA KURUDI KAZINI LAKINI BADO MADAKTARI BINGWA HAWAJAREJEA KAZINI KATIKA VITENGO VINGINE

No comments:

Post a Comment