|
Philipo Mulugo, Naibu Waziri Elimu na Ufundi |
|
Baadhi ya mabanda ya maonesho |
|
Geophrey Tenganamba, Mshiriki wa Maonesho Kutoka Perfect Path Innovators |
Naibu Waziri wa Elimu Philipo Mulugo amesema kuwa serikali imeanza mpango wake wa kufuta shule na vyuo ambavyo vimekua
vikifanya udanganyifu wa usajili na mitihani na kuahidi kuzisaidia taasisi za elimu zisizokuwa za kiserikali katika jitihada
za kuboresha elimu katika ngazi mbalimbali alipokuwa akifunga maonesho ya elimu ya siku mbili yaliyoandaliwa na kampuni ya Fayek katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya washiriki walikuwa ni shule za sekondari za Marumbo, Kenton, St. Mary's, St. Emmanuel, Baobab Girls, Chuo cha KAM, Techno Brain, Perfect Path Innovators, Tanzania Schools Directory, Oxford, Radar Education na Turn around Music Academy.
No comments:
Post a Comment