Monday, July 2, 2012

MGOMO WA MADAKTARI UNAENDELEA LIWALO NA LIWE





Siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka madaktari walio kwenye mgomo kurejea kazini na kuwahudmia wagonjwa, Madaktari Bingwa nchini wametangaza mgomo na kusema liwalo na liwe.

Mgomo huo ambao unaonekana kuwa wa kimaslahi zaidi unaonekana kushika kasi kila uchao tofauti na ilivyokuwa mwanzoni mwa wiki iliyopita.

Kiongozi wa Madaktari Bingwa Dr Catherine Mng’ong’o amewaambia waandishi wa habari Jijini Dar es salaam kuwa baada ya kikao chao cha Jumatatu, wamekubaliana kuendelea na mgomo wa nchi nzima.

Dr Mng’ong’o amesema, hawawezi kuendelea na kazi kwa vitisho vya serikali huku wenzao wakifukuzwa bila taratibu na hivyo wameamua kuendelea na mgomo wao.

Edwin Chitage ni katibu wa jumuiya ya madaktari nchini ambaye anasema wamesikitishwa na kauli hiyo ya Rais na kutaka suluhu ya mezani zaidi kumaliza mgogoro huo.

No comments:

Post a Comment