Chama Cha walimu Tanzania CWT
kimelaani taarifa za upotoshwaji kuhusiana na mgogoro baina yao na serikali
huku kikisisitiza kuwa hakitaanza mgomo hadi pale siku zilizoombwa kuongezwa na
kamati ya usuluhishi kumalizika.
Gracian Mukoba ni Rais wa CWT amezungumza na waandishi wa habari Jijini Dar
es Salaam na kusema kuwa bado wamekuwa wakiona umuhimu wa walimu nchini hivyo
serikali haina budi kusikiliza kilio chao.
Chama hicho awali kiliweka
bayana nia yake ya kuanza mgomo endapo serikali isingetimiza madai yake ya
msingi. CWT pia imekanusha taarifa za
kuwepo mgomo eneo lolote la Tanzania huku ikisisitiza kuwa hadi sasa umma na
walimu watambue kuwa hawaruhusiwi kugoma wala kushawishi kuwepo kwa mgomo
miongoni mwa walimu nchini.
No comments:
Post a Comment