Wednesday, June 20, 2012

Mabalozi wa Africa watoa msaada




Mabalozi 9 kutoka nchi za Afrika wametoa msaada wa dola elfu 6  na mia tano(shilingi za kitanzania milioni 10) kwa mke wa baba wa Taifa mama Maria Nyerere kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu waliopo butiama mkoani mara. Msaada huo utasaidia malazi kwa watoto hao ambao Mama Maria Nyerere aliwachukua na kuwapa hifadhi pamoja na kuwasomesha kutokana na mazingira magumu waliyokuwa wakiishi.
Mabalozi hao wametoa msaada huo jijini Dar Es Salaam wakati wa ziara waliyoifanya mkoani humo.

No comments:

Post a Comment