Saturday, July 28, 2012

WALIMU WATANGAZA MGOMO KUANZIA JULAI 30

Gratian Mkoba, Rais wa CWT


Gratian Mkoba akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari


Licha ya Serikali kuwataka walimu kusitisha mgomo kwa madai kuwa ni batili, Chama Cha Walimu Tanzania CWT kimetangaza kuanza kwa mgomo rasmi wa walimu nchi nzima kuanzia Julai 30, mwaka huu hadi serikali itakapotekeleza madai yao ikiwemo ongezeko la mishahara kwa asilimia 100.

Madai mengine ni Posho za kufundishia kwa walimu wa sayansi asilimia 55 na walimu wa masomo ya sanaa asilimia 50, na posho ya mazingira magumu asilimia 30 ambapo madai hayo yalishindwa kusuluhishwa na Tume ya usuluhishi.

Rais wa CWT Gratian Mukoba ametoa ufafanuzi kuhusiana na suala zima la kuanza kwa mgomo huo na kubainisha kuwa mgomo huo ni halali kutokana na kura za wanachama wake kufikia asilimia 95.7 ya idadi ya wanachama wote.

Mukoba amesema pia kuwa wamekuwa wakipata vitisho kutoka serikalini vya kuwataka kujaza fomu maalum za kutaka kujua iwapo wanaunga mkono mgomo huo au la!

Julai 25, mwaka huu jumla ya wanchama 183,000 wamepiga kura kupitia wawakilishi wa CWT 21500 nchi nzima ambapo wanachama 153,848 sawa na asilimia 95.7 wamepiga kura za kuunga mkono mgomo huo.

Julai 27 mwaka huu serikali kupitia ofisi ya katibu mkuu kiongozi imewataka waalimu hao kusitisha mgomo huo kwani shauri hilo tayari lipo mahakama kuu divisheni ya kazi na kuwataka kuupuza mgomo huo na kuendelea na kazi kama kawaida.

No comments:

Post a Comment