![]() |
Habib Juma akipokea msaada wa baisikeli |
![]() |
Alex Msama - Mkurugenzi Msama Promotions |
![]() |
William Dahani mmoja wa waliopokea msaada huo |
Wafanyabiasha na watanzania kwa ujumla wametakiwa kuendelea
kuwasaidia watu wenye ulemavu ili waweze kujikimu na kutambua kuwa wana nafasi kubwa ya kuwasaidia watua hao
katika masuala mbalimbali.
Wafanyabiashara hao wametakiwa kutenga muda wao na
kuwafikiria zaidi watu wenye ulemavu kuwasaidia kwa hali na mali kwani baadhi
yao wamekuwa wakikata tamaa kutokana na ugumu wa maisha uliopo.
Akizungumza wakati wa kutoa msaada wa baiskeli kwa baadhi ya
watu wenye ulemavu mkurugenzi wa kampuni ya msama promotion Alex Msama amesema
kuwa kuna umuhimu mkubwa katika kuwasaidia watu hao na ndiyo maana kampuni yake
ikahamua kutoa msaada huo.
Nao Habibu Juma na William Dahani, waliopata msaada huo, wameitaka jamii
kuguswa na watu hao na kuwasaidia katika masuala mbalimbali
Watu hao wenye ulemavu wamekuwa wakihitaji misaada ya aina
mbambali ikiwemo fedha, elimu, na ushauri ili waweze kupata nafuu ya ugumu wa
maisha unaowakabili baadhi yao.
No comments:
Post a Comment