Saturday, July 28, 2012

WATANZANIA WAPOKEA VIZURI PUNGUZO LA GHARAMA ZA KUUNGANISHA UMEME

Nguzo ya umeme iliyofungiwa transfoma
Baadhi ya wananchi wameipongeza serikali kuazimia kupunguza gharama za uunganishwaji umeme, huku wengine wakitaka huduma hiyo kuwa bure kama inavyofanyika katika mataifa mengine.

Maoni hayo yamefuatia tamko la Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo kutangaza bungeni jana kuwa kuanzia January mwakani punguzo la kuunganishiwa umeme litashuka kwa 68.11% vijini na mijini kwa 29.48%.

Kutokana na mwamko wa wananchi kufuatilia mjadala wa moja kwa moja katika bunge la bajeti kwa 2012/2013, suala la umeme limezua mjadala kwa raia wengi wakiwa sehemu zao za kazi. Katika kona mbalimbali za jiji la Dar es Salaam wajasiriamali mbalimbali wameonyesha kuwa kilio chao sio katika gharama za uunganishwaji umeme, bali wana hofu ya maneno mengi ya serikali.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizokosa fursa ya kushamiri kiviwanda kutokana na uhaba wa huduma za umeme alieleza bwana Deogratias Kishombo ambaye ni mhariri wa habari za biashara na uchumi kutoka gazeti la The african.

Dennis Mwasalanga

No comments:

Post a Comment