Saturday, July 28, 2012

CD FEKI ZA WASANII WA MUZIKI WA NJILI ZANASWA PAMOJA NA MITAMBO INAYOTUMIKA KUZITENGENEZA

CD/DVD feki
Operesheni Maalum ya kuwasaka wafanyabiashara wasio waaminifu wanaodurufu kazi za wasanii wa muziki wa Injili imenasa mitambo na cd feki vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 25.

Operesheni  hiyo imewakamata  wakazi 8 wa jiji la Dar s Salaam wakiwa na cd mbalimbali za muziki wa Injili huku wakitaraji kuonyesha mitambo ambayo imekuwa ikitumika kurudufu kazi hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Slaam mara baada ya zoezi hilo la kubaini wafanyabiashara hao Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Auction Mart Alex Msama amesema kuwa jitihada za operesheni hiyo zina lengo la kuondoa kabisa wafanyabiashara wanaodhurumu haki ya wasanii.

Msama amesema kuwa zoezi hilo ambalo limeungwa mkono na COSOTA litahakikisha kuwa linakuwa endelevu huku akiwataadharisha wale wote wanawatumia wafanyabiashara wadogowadogo kufanya biashara hiyo ambayo inawanyima haki wasanii wa muziki wa injili nchini kwani wamekuwa hawafaidiki na kazi wanazozifanya.

Kumekuwa na baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakipitisha katika mitaa mbalimbali  kazi za wasanii nchini na kuziuza  kwa bei ya chini  kinyume cha sheria jambo linalowanyima haki wasanii wengi nchini.

No comments:

Post a Comment