Sunday, July 1, 2012

CWT yakumbushia mgomo



Gratian Mkoba akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari



Chama cha walimu Tanzania CWT kimesema kinaamini kuwa serikali itatekeleza uamuzi waliokubaliana kabla ya tarehe 10 mwezi huu la sivyo Chama hicho kitaanza mgomo nchi nzima kushinikiza madai yao kutekelezwa

Chama hicho kilitangaza mgogoro na serikali tangu june 8 mwaka huu kwa kile walichoeleza kuwa Serikali imepuuza madai yao yakiwemo ongezeko la mshahara kwa asilimia mia moja pamoja na kuboreshewa mazingira ya kazi

Rais wa CWT  Gratian Mukoba amekutana na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam na kuelezea azma yao hiyo, kubwa ikiwa ni kuweka sawa taarifa kuwa walimu hawataanza mgomo mpaka pale serikali itakapotoa majibu tarehe 10 ya mwezi huu

Wakati Chama cha walimu kikiweka bayana uamuzi wa kufanya mgomo endapo Serikali haitakuja na majibu ya hakika kwao, wapo baadhi ya walimu wametuhumiwa kutumiwa kujenga makundi miongoni mwao na hivyo kutishia kukwamisha upatikanaji wa madai yao ya muda mrefu

No comments:

Post a Comment