Wednesday, June 27, 2012

Vyuo vyote nchini kutoza ada kwa Shilingi za kitanzania sasa


Prof. Mchome, Mkurugenzi wa TCU

Mkurugenzi wa TCU, Prof. Mchomi amesema vyuo vya Kampala International University (Dar es salaam) na IMTU ambavyo vilikuwa vikitoza ada za masomo kwa Dola za kimarekani, vitaanza kutoza ada hizo katika shilingi za kitanzania kuanzia mwaka wa masomo 2012/13.

Ameyasema hayo katika mkutano na waakilishi wa serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu nchini. Kuhusu migogoro na migomo ya vyuo hivyo amesema hatua za kisheria zitachukuliwa kuviwajibisha vyuo vinavyojiendesha kiholela.

No comments:

Post a Comment