Saturday, July 7, 2012

JAJI OTHMAN CHANDE AWATUNUKU MAWAKILI 286







JAJI Mkuu wa Tanzania Chande Othaman jana aliwaapisha na kuwatunuku leseni za kufanya kazi mawakili wa kujitegemea 286 na kuwataka waende vijijini kuwasaidia watanzania.

Kuapiashwa kwa mawakili hao wapya kunaongeza idadi ya mawakili kutoka 2316 waliokuwepo na kufikia 2602.

Baada ya kuwatuniku mawakili hao Jaji Chande amesema ipo haja kwa mawakili hao kujikita kwenye maeneo ya pembezoni ambayo yana idadi kubwa ya watanzania wenye mahitaji mengi ya kisheria.

Pia Jaji mkuu huyo ametoa wito kwa waliojiandikisha kuwa mawakili lakini hawajasajiliwa wafike Baraza la Elimu ya Sheria liwasajili na hatimaye kuapishwa na kuwa mawakili kamili hali itakayosaidia kuongeza idadi ya mawakili nchini.

No comments:

Post a Comment